Saturday, March 16, 2024

WANANCHI MANISPAA YA SINGIDA WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO ZOEZI LA UHAKIKI...


WIZARA ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, imewagiza Watendaji wa vijiji, kata na mitaa katika halmashuri ya Manispaa ya Singida kuliweka katika agenda ya kudumu kwenye vikao vya Kamati za Maendeleo za Kata (WDC) suala la anwani ya makazi ili kuweka uendelevu wa usimamizi na uhakiki wa taarifa za anwani za makazi na kuwasihi wakazi wa Manispaa ya Singida kutoa ushirikia ili kufanikisha uhakiki huo sanjari na taarifa zao kuingizwa katika mfumo wa anwani za makazi. Mtaalamu wa Mfumo wa anwani za makazi kutoka Wizara hiyo, Innocent Jacob, amesema hayo (Machi 15, 2024) wakati wa mafunzo ya siku mbili ya Uhakiki Anwani za Makazi katika Mfumo wa Kidigitali (NaPA) yanatolewa kwa watendaji wa Kata, Vijiji na Mitaa na Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida kwa ajili ya uhakiki wa anwani za makazi. Jacob amesema anwani za makazi ni muhimu sana kwasababu zinasaidia ulinzi na usalama,kutoa huduma kwa wakazi na pia inasaidia biashara mtandao kupitia fumo wa Kidigitali (NaPA). Kwaupande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Adrianus Kalekezi, amewaagiza Watendaji wa Kata vijiji na wenyeviti wa mtaa kutekeleza kikamilifu zoezi hilo na kutoa taarifa kwa wakati katika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ili kujua kila hatua ya utekelezaji. Naye Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Mtaa katika Manispaa ya Singida Abilai Hussein,ambaye ni Mwenyekiti wa Mji wa zamani amewasihi wenyeviti wenzake kuunga mkoano juhudu za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuhakikisha wananchi wanahamasishwa kwa kushiriki kikamilifu utoaji taarifa sahihi ili kuhakikiwa na kuwekwa katika mfumo wa anwani za makazi.

Mafunzo yakiendelea.


Tuesday, March 12, 2024

RC DENDEGO APOKELEWA KWA KISHINDO MKOANI SINGIDA NA KUKADHIWA RASMI OFISI

Mkuu mpya wa Mkoa wa Singida Halima Dendego, ameahidi kusimamia shughuli za maendeleo kwa niaba ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, na kutoa tahadhari kwamba kwenye uongozi wake hataki kusikia suala la msamiati wa changamoto kama sababu mojawapo ya kukwamisha maendeleo.

Dendego amesema hayo muda mfupi alipokabidhiwa ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Peter Serukamba, na kuzungumza na Watumishi wa ofisi hiyo, Kamati ya Ulinzi na Usalama, Viongozi wa vyama vya siasa, Viongozi wa Dini na wageni waalikwa mbalimbali.

"Nimekuja Singida kupokea majukumu ya kazi niliyopewa na Mheshimiwa Rais wa Hamguri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan, kama alivyoacha kaka yangu Serukamba, na mimi nitasimamia ili tupige hatua mbele zaidi, nawahakikiahi kama aliyeondoka ni Kulwa, basi aliyekuja ni Doto...lazima kazi ziendelee kwa ajili ya kuleta maendeleo." alisema Dendego.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego (kushoto) akipokelewa na vijana wa skauti mara baada ya kuwasili katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida kwaajili ya makabidhiano na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Peter Serukamba(hayupo pichani).

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amesema ni lazima kazi zifanyike na majibu yapatikane katika utumishi wake huku akaisisitiza kuwa atakuwa msikivu mnyenyekevu na mtulivu kwa anaowaongoza na kusimamia shughuli na miradi ya maendeleo mkoani Singida.

Amewahakikishia utumishi uliotukuka na ushirikiano wa dhati watumishi wote wa Mkoa wakiwemo wakuu wa Wilaya za Mkoa, Wakurugenzi wa Halmashauri ili kuwaletea maendeleo ya dhati wananchi na Watanzania kwa ujumla wa Mkoa wa Singida.

Akizungumza kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Singida, Katibu Mwenezi wa chama hicho pamoja na kuwapongeza wakuu hao wa mikoa, alisema CCM itaendeleza ushirikiano wa dhati na Serikali ya Mkoa kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba, akizungumza na viongozi na baadhi ya wananchi walioshiriki katika hafla ya makabidhiano ya ofisi yalifofanyika leo Machi 12, 2024 mkoani Singida.

Awali aliyekuwa Mkuu wa Mkoa aliyehamishiwa mkoani Iringa, Peter Serukamba, alitumia fursa hiyo kuzishukuru kada mbalimbali za uongozi tangu awasili mkoani Singida mwaka mmoja na miezi saba iliyopita na kufafanua kuwa amejifunza mengi ya maendeleo akiwa Singida.

Serukamba alisema akiwa Singida anajivunia kupandisha matumizi ya mbolea ikilinganishwa na hali aliyoikuta huku pia akifanikisha upatikanaji wa mbegu ya ruzuku kwa zao la alizeti.

Serukamba alisema pia katika kipindi chake mkoani Singida anajivunia kumaliza tatizo la mauaji lililokuwa linaikabili Wilaya ya Manyoni kutokana na kukithiri kwa mauaji nyakati za usiku na ufukuaji wa makaburi kutokana na imani za kishirikina.

Amesema kwa nguvu hiyo hiyo, ndiyo atakayoenda nayo Iringa, kwa lengo la kupambana na kuongeza juhudi ili asiyashushe maendeleo ya mkoa huo yaliyochagizwa na Mkuu wa Mkoa Halima Dendego, aliyehamishiwa sasa mkoani Singida.

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Singida, Katibu mwenezi wa CCM, Elphas Lwanji amesema kuwa, chama hicho kinaahidi kushirikiana na Serikali ya Mkoa huo kupitia uongozi wa Halima Dendego, kama ambavyo walimpatia Peter Serukamba.

Mkuu mpya wa Mkoa wa Singida Halima Dendegoakizungumza na viongozi na baadhi ya wananchi walioshiriki katika hafla ya makabidhiano ya ofisi yalifofanyika leo Machi 12, 2024 mkoani Singida.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba, akimkabidhi taarifa ya Mkoa wa Singida kwa Mkuu wa Mkoa huo Halima Dendego, wakati wa hafla ya makabidhiano ya ofisi.

Wakuu wa Mikoa wakiweka saini katika vitabu vya makabidhiano ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida Machi 12, 2024























Saturday, March 09, 2024

SERUKAMBA AWAAGA WATENDAJI MKOANI SINGIDA KWA KUWAAGIZA MIRADI YOTE KUKAMILIKA KWA WAKATI

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, leo tarehe 9 Machi, 2024 amehamishiwa kutoka Mkoa wa Singida kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringia na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Halima Omar Dendego, kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida huku akiwaagiza watendaji kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati.

Kwa muujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 09 Machi, 2024 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses M. Kusiluka ambaye ni Katibu Mkuu Kiongozi, ikieleza mabadiliko madogo ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri imeeleza kuwa uteuzi na uhamisho huo unaanza leo tarehe 09 Machi, na uapisho wa Wakuu wa Mikoa utapangwa baadaye. 

Akiwa katika kikao cha kamati ya ushauri wa Mkoa (RCC) kilichofanyika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Singida Serukamba, ghafla alionyesha tabasabu na shahuku ya kuongea jambo huku wajumbe nao wakionesha tabasabu kwa kile kilichokuwa kimesambaa kwenye mitandao ya kijamii kikihusisha uteuzi na uhamisho huo.

Mara baada ya muda mfupi ndipo Serukamba aliposhindwa kuvumilia na kuamua kuwaambia wajumbe wa kikao hicho kwamba amehamishwa kutoka Mkoa wa Singida na kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Halima Omar Dendego, kuhamia Mkoa wa Singida.

Aidha, Serukamba, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kumuamini katika nafasi hiyo na amemuahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii katika kuhakikisha anawatumikia Wananchi hao wa Mkoa wa Singida kikamilifu.

Hata hivyo Serukamba, amewashukuru Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Singida, akianzia na Katibu Tawala Mkoa huo Dkt. Fatuma Mganga kwa ushirikiano aliyokuwa akiupata, watumishi wote wa Sekretarieti ya Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya, Wakurugenzi, Viongozi wa Dini pamoja na Wananchi wote kwa ujumla.

Katika hatua nyingine, wajumbe wa kikao hicho wamempongeza aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo kwa katika kipindi chote cha uongozi wake Mkoani hapo wakisema hakika amekuwa ni kiongozi aliyekuwa akisukuma maendeleo ya mtu mmoja mmoja na wanasingida kwa ujumla hasa katika suala la kilimo cha utumiaji mbolea.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, akionyesha tabasabu lake muda mfupi mara baada ya kuonekana kuendelea kuaminiwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa wakati alipokuwa kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC).









Friday, March 08, 2024

WANAWAKE MKOANI SINGIDA WAHAMASISHWA KUJITOKEZA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI YAFANA MKOANI SINGIDA

MKE wa Waziri Mkuu Mstaafu,Tunu Pinda ameitaka ,Serikali, wadau wa maendeleo, taasisi za Serikali na wananchi kwa ujumla   mkoani Singida kuchukua hatua za makusudi kushughulikia masuala ya ubaguzi wa kijinsia na uonevu wanavyofanyiwa Wanawake. 

Wito huo ameutoa leo Machi 8, 2024 wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kimkoa wilayani Ikungi mkoani hapa ikiwa na kauli mbiu ya wekeza kwa mwanamke kuharakisha maemdeleo ya taifa na ustawi wa jamii.
Pinda alisema Tanzania inaunga mkono jitihada za kimataifa za kukuza usawa wa kijinsia  ikiwa ni pamoja na kujielekeza katika utekelezaji wa mikakati ya kufikia kizazi chenye usawa.

Alisema Serikali katika kutekeleza hilo imezindua Kamati ya ushauri ya Kitaifa ya utekelezaji wa ahadi za nchi kuhusu kizazi chenye usawa uliofanyika tarehe 16 Disemba, 2021 Jijini Dodoma ambapo Mgeni rasmi alikuwa rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Alisema kuanzishwa kwa kamati hiyo ni jitihada za Serikali katika kutoa msukumo wa utekelezaji wa masuala ya haki na usawa kwa wanawake na wanaume.

Nachukua nafasi hii kumpongeza Mwanamama, Amiri Jeshi Mkuu, na Raisi Dk. Samia Suluhu Hassan kwa uhodari wake wa kufanya kazi kubwa ya kuleta mabadiliko kila sekta nchini katika kuleta miradi ya maendeleo endelevu, kila mkoa hadi wilaya, kata na hata mtaa na sisi wanawake tukiwa ni wanufaaika wakubwa wa Maendeleo haya,"alisema Pinda.

Aidha, aliwapongeza wanawake wote nchini na hususani wanawake wa Mkoa wa Singida kwa upambanaji, wajasiri na hodari kwa kuchapa kazi.

Alisema lengo kuu la kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ni kutoa fursa kwa jamii kupima utekelezaji wa maazimio, matamko, mikataba na itifaki mbalimbali za kimataifa, kikanda na kitaifa zinazohusu masuala ya maendeleo ya jinsia na uwezeshaji wanawake. 

Alisema kufanya hivyo ni kuhakikisha kuwa haki za wanawake kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na kisiasa zinapatikana na zinalindwa.

"Kuadhimisha siku ya wanawake duniani ni kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kutambua na kuthamini uwezo na mchango mkubwa wa wanawake katika kuleta maendeleo pamoja na kuelezea jitihada mbalimbali zilizofanywa na serikali na wadau mbalimbali katika kuwajengea uwezo wa kiuchumi na kijamii ili waweze kushiriki kikamilifu katika kujiletea maendeleo yao, familia zao, jamii na Taifa kwa ujumla," alisema Pinda.

Alisema kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu inaendana na jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuwekeza kwa wanawake kiuchumi, Kijamii, Kiafya, Elimu, Michezo na Utamadumi.hivyo ni wajibu kwa wanawake kutambua hilo na kumuunga mkono Rais kwa juhudi kubwa anazozifanya katika kuwezesha wanawake,na kuleta mabadiliko kila sekta nchini katika kuleta Miradi ya maendeleo endelevu.

Aliongeza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Mendeleo Jamii Jinsia,Wanawake na Makundi Maalumu, inayoongozwa na Mwanamama, Doroth Gwajima  inadhamini na kuwatambua umuhimu wa wanawake wote na wajasiriamali ni miongoni mwa watu muhimu katika kukuza uchumi wa mtu moja moja na Pato la Taifa. 

"Nitoe rai kwa Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri kutenga eneo maalumu katika masoko yao kwa ajili ya malezi yaani Day care Center ili kuwezesha wanawake wajasiriamali wenye watoto waweze kupata sehemu maalumu ya kunyonyesha na watoto kupata muda wa kucheza, hali hii itaboresha zaidi malezi na makuzi ya Awali ya Watoto na kuimarisha usalama wao," alisema Pinda.

Kwaupande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, amesema siku ya Mwanamke Duniani ni siku ya kutazama na kutafakari juu ya nafasi ya Mwanamke katika suala zima la maendeleo. ni siku ya kujipima na kutathimini namna gani wanawake wamewezeshwa kujitambua na kushirikishwa katika mipango ya maendeleo ya jamii kwa kushirikiana na wanaume.

"Kwa namna ya pekee katika kusheherekea siku hii sisi wanasingida tunataka kumuelezea mwanamke Jasiri muongoza njia, shupavu na mfano bora wa kuigwa sio tu na kila mwanamke bali kila mtanzania bila kujali ni mwanamke au mwanaume. Mwanamke huyo ni: Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan". Amesema RC Serukamba

















Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba (kushoto) akisalimiana na Mgeni rasmi Mama Tunu Pinda wakati wa Maadhimisho hayo.